@SikilizaTogolan Profile picture

SikilizaTogolani

@SikilizaTogolan

Kila Mtu kwa KARAMA yake, KADRI yake na KUDRA yake!

Similar User
AyoTV photo

@ayotv_

Joramu Nkumbi photo

@NkumbiJoram

Radio Maria Tanzania photo

@radiomariatz

Tanzania Abroad TV photo

@AbroadTanzania

OscarOscar photo

@mzeewakaliua

Togolani Mavura photo

@tonytogolani

Mark J. Mwandosya photo

@MarkMwandosya

BBC News Swahili photo

@bbcswahili

mwaisa_mtumbad photo

@Nyonyoma1

Peter Madeleka photo

@PMadeleka

Wizara ya Afya Tanzania 🇹🇿 photo

@wizara_afyatz

Samia Suluhu photo

@SuluhuSamia

Fortunatus Buyobe photo

@fbuyobe

Salim Kikeke photo

@Salym

Nikkwapili photo

@nikkwapili

"Kama tunao uwezo wa kuiona nia njema tunapokosewa na wale tunaowapenda, basi tunao uwezo pia wa kuiona nia njema tunapokosewa na wale tusiowapenda au wasiotupenda. Tukibadili mtazamo wetu na vile tunavyovitazama hubadilika pia." ~Togolani Mavura

Tweet Image 1

"Katika kurekebisha kwangu kunaweza kusababisha mtikisiko na hata nyufa kwako. Si kwamba nimedhamiria kukutikisa bali ni kwasababu uko karibu sana na mimi. Ungekuwa mbali nisingekufikia. Ndio ilivyo kwenye maisha, ukiona unakereka na mtu huenda tatizo ni wewe umemsogelea sana."

Tweet Image 1

"Wajibu wa wazazi/walezi ni kukutoa kizani hadi kwenye njia panda ya ufahamu, kuanzia hapo maisha yako ni matokeo ya machaguo yako mwenyewe." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Katika ugomvi, ogopa sana kumfikisha mgomvi wako umbali ambao huwezi kuufikia kumpa mkono wa kumrudisha." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Wewe ni muhimu kwa wale unaowafaa. Usihamishie umuhimu wako kwa wengine. Hao wengine kabla hujawataka wakupe umuhimu uliozoea kuupata, wape nao fursa ya kuuona huo umuhimu wako waliouona hao wengine katika maisha yao." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Maisha yetu ni kuitafuta maana. Maana ya uwepo wetu duniani, maana ya hatma yetu duniani, maana ya masuala mengine kama rizki, mapenzi na furaha, hali kadhalika, maana ya kukosa na maana ya kupata. Maana ndio masumbuko yetu makuu na wanaotupa maana wanayakamilisha maisha yetu!"

Tweet Image 1

"Baada ya kitasa cha mlango wa maisha kubadilishwa, elimu siku hizi haipaswi tena kuwa ufunguo wa maisha bali inapaswa kuwa namba ya siri." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Kila tunapothubutu tunajisogeza mbali na uwezekano wa kushindwa, bila kuthubutu tunajipa uhakika wa kushindwa." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Sababu unazotumia kuhalalisha kushindwa kwako ndio zinazotumika kama motisha kwa upande wa mwenzako. Mitazamo yetu hutujenga na hutubomoa." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Kazi ni Ibada." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Hakuna lisilowezekana, lakini lipo usiloweza. Kuliko kupoteza muda kwa usiloliweza, hamishia nguvu zako kwanza kwa lile unaloliweza." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Usifadhaishwe na udogo wako, usiaminishwe kuwa udogo wako ni hali ya kudumu.Udogo ni msingi wa kuanzishia kikubwa, mbegu zote ni ndogo ikilinganishwa na mazao yatokanayo na mbegu zake. Huwezi kuukumbatia mbuyu kwa ukubwa wake,lakini mbegu ya mbuyu haijai mkononi kwa udogo wake."

Tweet Image 1

"Ogopa sana watu wanaokaa kimya huwa ni wazuri sana wa kuhifadhi kumbukumbu." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Kila pakacha na mzigo wa uzito wake, kila kifua na kiwango chake cha kubeba na kuhifadhi mambo. Jua kiasi chako, usijilinganishe na mwenzako. Jepesi lake laweza kuwa kubwa lako." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Kama tunaamini Mungu ndie mtoa rizki, na tunaamini hamna nguvu ya kuzuia alitakalo, na kuwa ulipata kwa sababu aliwazuia wasiotaka usipate, basi ukikosa jua ana makusudi ya kuwaacha wasiotaka upate wafanikiwe usipate. Tushukuru Mungu kwa kila jambo. Kupata na kukosa kuna Mungu!"

Tweet Image 1

"Kiwango cha ujasiri walichopata kumsimulia yeye namna wasivyokupenda wewe ndio kinachopaswa kukustua zaidi kuliko kile walichokisema. Ama yeye ni mmoja wao, ama anafanana nao,au alionekana kutobugudhika na kusemwa kwako kiasi kwamba hawakuogopa kuendelea kumsimulia kuhusu wewe."

Tweet Image 1

"Ili tusi litimie lazima awepo wa kutukanika. Kama wa kutukanika hayupo na tusi halipo. Thamani ya tusi ni kule kuamshwa nyongo ya anayetukanwa. Tusi bila ya kuamsha nyongo ni kama 'kivumishi' tu. Hatuwezi kuzuia watu kututukana, ila tunaweza kujizuia kutukanika. Mpuuzi Mpuuzie."

Tweet Image 1

"Si kila mwanga ni nuru. Mwanga mwingine unaumiza macho na kupofusha." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

"Binadamu wengi huvithamini vitu vyao pale wanapoingiwa wasiwasi wa kuvipoteza au pale wengine wanapoonyesha hali ya kutaka kufika bei. Vigezo na masharti hayo hayo ndio hutumika kututhaminisha katika maisha ya wengine. Hakikisha wakati wote hutoki nje ya bei elekezi ya soko!"

Tweet Image 1

"Ziko nyakati katika maisha unaletewa malaika na ziko nyakati unaletewa adui. Ukiletewa malaika kamata mikono yake akuvute uinuke. Ukiletewa adui, kanyaga mabega yake ukwee juu. Daima mwendo ni kwenda juu aje malaika aje adui, iwe ni kutumia mkono au mabega." ~Togolani Mavura.

Tweet Image 1

This account does not follow anyone
Loading...

Something went wrong.


Something went wrong.